Thamani Trust Logo

THAMANI TRUST FOUNDATION

Jukwaa Salama la Kuunganisha Waajiri, Wafanyakazi na Wakala

Tunaimarisha heshima na thamani ya dada wa kazi kwa usajili, uhakiki wa taarifa, na uratibu wa ajira unaozingatia utu.

Wafanyakazi Walioidhinishwa
5
Maombi ya Kazi
6
Wakala
1
Placements
2

Huduma Muhimu

Chagua huduma unayohitaji na anza hatua inayofuata.

Wafanyakazi Waliopendekezwa

Walioidhinishwa na tayari kwa ajira.

Tazama wote
Sarah alfa

Sarah alfa

Tabora

Ujuzi utaongezwa baadae
Muombe Huyu
Beatrice daniel

Beatrice daniel

Mkoa haujawekwa

Ujuzi utaongezwa baadae
Muombe Huyu
Sara mbena

Sara mbena

Mbeya

Ujuzi utaongezwa baadae
Muombe Huyu
omega jirani

omega jirani

singida

usafi mapishi
Muombe Huyu
mary didas

mary didas

tabora

malezi ya watoto
Muombe Huyu

Jinsi Inavyofanya Kazi

Mchakato mfupi, wazi na salama kwa mwajiri, mfanyakazi na wakala.

1

Sajili/Tuma Ombi

Waajiri hutuma mahitaji, wafanyakazi na mawakala hujisajili rasmi.

2

Uhakiki wa Taarifa

Timu inahakiki nyaraka, wadhamini na sifa kabla ya kuidhinisha.

3

Ulinganifu na Ufuatiliaji

Tunafanya matching, usimamizi wa ajira na ulinzi wa maslahi ya pande zote.

Programu Kuu za Thamani Trust

Muhtasari wa programu zinazounda kampeni ya Sauti ya Thamani.

Programu zote

Haki na Ulinzi

Utambulisho na Ulinzi wa Haki za Dada wa Kazi

Programu hii inajenga mfumo rasmi wa usajili, mikataba halali, malipo salama, bima ya afya na utatuzi wa migogoro ili dada wa kazi wafanye kazi kwa usalama, heshima na ulinzi wa kisheria.

Usajili rasmi na kadi za utambulisho Mikataba ya kazi iliyo wazi na halali Bima ya afya, hifadhi ya jamii na stahiki Kupokea malalamiko, usuluhishi na rufaa
Soma programu

Elimu na Mafunzo

Dada wa Kazi Mwenye Thamani

Warsha hizi zinawapa dada wa kazi ujuzi wa kazi za nyumbani, maadili ya kazi, malezi ya watoto, mawasiliano bora na mwelekeo wa maisha ili wawe wafanyakazi wenye weledi na kujiamini.

Usafi, utunzaji wa nyumba na usalama wa kazi Malezi bora ya watoto na afya ya familia Mawasiliano, nidhamu na udhibiti wa migogoro Vyeti vya ushiriki kwa wahitimu wa mafunzo
Soma programu

Uwezeshaji

Maisha, Akiba na Mwelekeo wa Baadaye

Programu hii inaandaa dada wa kazi kujitegemea kiuchumi kupitia elimu ya fedha, akiba, stadi za maisha, afya ya akili na maandalizi ya njia mbadala za kipato baada ya ajira.

Elimu ya fedha, matumizi na akiba Maamuzi sahihi ya maisha na kujitambua Stadi za maisha, uthabiti wa kihisia na afya ya akili Ujasiriamali mdogo na miradi ya kipato
Soma programu

Kampeni ya Kitaifa

Sauti ya Thamani

Hii ni kampeni ya kitaifa ya kubadili mitazamo ya jamii kuhusu dada wa kazi kupitia elimu ya jamii, vyombo vya habari, mitandao ya kijamii na ushiriki wa viongozi wa mitaa, dini na taasisi mbalimbali.

Elimu kwa waajiri, familia na wazazi Vipindi vya redio, TV na kampeni za kidijitali Uhamasishaji wa viongozi wa dini na serikali za mitaa Kupaza sauti dhidi ya unyanyasaji na unyanyapaa
Soma programu

Wiki ya Kitaifa

Wiki ya Dada wa Kazi Kitaifa

Programu ya kila mwaka ya siku saba inayotambua mchango wa dada wa kazi kupitia uzinduzi rasmi, elimu ya jamii, sanaa, ushuhuda, majadiliano ya sera na utoaji wa tuzo za kitaifa.

Siku 7 za elimu na uhamasishaji wa kitaifa Ushuhuda, sanaa na majukwaa ya jamii Majadiliano ya sera na ushiriki wa wadau Tuzo za Thamani kwa dada wa kazi na waajiri bora
Soma programu

Machapisho ya Hivi Karibuni

Miongozo, nyaraka na maarifa ya kuendeleza ajira zenye hadhi.

Angalia yote
Misingi ya Heshima kwa Dada wa Kazi

Misingi ya Heshima kwa Dada wa Kazi

Somo hili linaeleza misingi ya utu, mawasiliano sahihi na mazingira salama ya kazi za ndani.

1

Soma zaidi

Wadau na Washirika

Tunashirikiana na taasisi za kijamii, wadau wa ajira na viongozi wa jamii kuimarisha mfumo salama wa ajira kwa dada wa kazi.

Tazama Ushirikiano
Halmashauri
Asasi za Kiraia
Mashirika ya Dini
Vikundi vya Jamii

Anza Hatua Leo

Iwe unahitaji mfanyakazi, unataka kujiunga kama mfanyakazi, au ungependa kuunga mkono shughuli zetu, jukwaa letu liko tayari.