THAMANI TRUST FOUNDATION
Kuinua Hadhi na Thamani ya Dada wa Kazi Tanzania
Thamani Trust Foundation ni taasisi isiyo ya kiserikali yenye makao Dodoma, inayosimamia harakati ya kutambua, kulinda na kuendeleza ustawi wa dada wa kazi kupitia usajili rasmi, elimu, ulinzi wa haki na ushirikiano wa kimkakati na wadau mbalimbali.
Jina la Taasisi
Thamani Trust Foundation
Eneo
Dodoma, Tanzania
Aina ya Taasisi
Isiyo ya Kiserikali
Kampeni Kuu
Sauti ya Thamani
Utangulizi
Katika familia nyingi za Kitanzania, dada wa kazi ni nguzo muhimu isiyoonekana: wanatunza watoto, wazee, usafi wa nyumba, na utulivu wa kaya. Licha ya mchango huu, wengi wao hupitia mazingira magumu ya kazi bila mkataba, bila malipo ya wakati, bila ulinzi wa afya, na bila heshima wanayostahili.
Thamani Trust Foundation imeanzishwa kubadili hali hii kwa vitendo. Tunafanya kazi ili kazi za ndani zitambuliwe kama ajira rasmi yenye hadhi, stahiki na ulinzi wa kisheria, huku tukijenga uwezo wa kiuchumi na kitaaluma kwa dada wa kazi.
Takwimu za Mfumo
Wafanyakazi Walioidhinishwa
5
Maombi ya Kazi
6
Wakala
1
Placements
2
Changamoto Tunazoshughulikia
Ukosefu wa mikataba na ulinzi wa ajira
Wengi hufanya kazi bila mkataba rasmi, hivyo kukosa kinga ya kisheria na usalama wa ajira.
Mishahara kuchelewa au kukatwa kiholela
Kuna matukio ya malipo kucheleweshwa, kushikiliwa, au kufukuzwa bila stahiki.
Huduma duni za afya na bima
Wengi hukosa bima ya afya na fidia za madhara ya kazi, jambo linaloongeza hatari ya maisha.
Ukosefu wa mafunzo na kujiendeleza
Fursa chache za elimu na ujuzi mpya husababisha kudumaa kwa kipato na maendeleo ya maisha.
Dhamira
Kuwezesha na kuinua hadhi ya dada wa kazi kwa kuwatambua rasmi, kulinda haki na stahiki zao, kuwapa nafasi ya kujifunza na kujiendeleza, na kubadili mtazamo wa jamii kuhusu kazi za ndani kuwa kazi yenye heshima na mchango wa kitaifa.
Maono
Kujenga jamii yenye mfumo wa heshima, ulinzi na thamani kwa dada wa kazi, ambapo kila mfanyakazi wa majumbani anatambulika rasmi, anapata haki zake, na anathaminiwa kama nguzo ya maendeleo ya familia na taifa.
Makundi Yanayolengwa
4.1 Dada wa Kazi
- - Utambulisho rasmi na vitambulisho vya kitaasisi.
- - Ulinzi wa haki: mikataba, malipo sahihi, mapumziko, na usalama kazini.
- - Mafunzo ya weledi: malezi, usafi, mapishi, maadili, fedha na maisha.
- - Uwezeshaji wa kiuchumi: vikundi, akiba, mikopo midogo na miradi.
- - Kampeni ya heshima na hadhi ya kitaaluma kupitia vyeti na mitandao.
4.2 Waajiri
- - Elimu ya ajira bora: stahiki, mikataba, malipo na wajibu wa mwajiri.
- - Uhamasishaji wa heshima na utu kwa wafanyakazi wa majumbani.
- - Matumizi ya mfumo wa kidijitali kwa usimamizi wa taarifa na stahiki.
- - Kuzuia migogoro kwa kufuata taratibu za kazi na mawasiliano bora.
- - Kuwajenga waajiri kuwa mabalozi wa heshima ya kazi za ndani.
Programu Kuu
Utambulisho na Ulinzi wa Haki za Dada wa Kazi
Dada wa Kazi Mwenye Thamani
Maisha, Akiba na Mwelekeo wa Baadaye
Sauti ya Thamani
Wiki ya Dada wa Kazi Kitaifa
Matokeo Yanayotarajiwa
Utambulisho na Heshima Kuongezeka
Dada wa kazi kutambulika rasmi na jamii kuacha mtazamo wa dharau.
Ulinzi wa Haki na Stahiki
Malipo ya wakati, kupungua kwa unyanyasaji, na mifumo rasmi ya fidia.
Uwezo wa Kiuchumi
Ujuzi wa fedha, miradi midogo, na upatikanaji wa fursa za mikopo.
Ubora wa Huduma Majumbani
Weledi wa kazi, malezi bora ya watoto, na mazingira salama ya huduma.
Mabadiliko ya Mitazamo
Jamii kuona kazi za ndani kama taaluma yenye mchango halisi wa kitaifa.
Mitandao Imara na Sauti ya Pamoja
Vikundi vya dada wa kazi kushiriki mijadala ya sera na maamuzi ya maendeleo.
Hitimisho
Sauti ya Thamani ni harakati ya kimkakati ya kuokoa utu, kuimarisha ulinzi wa haki, na kuonyesha mchango wa dada wa kazi katika maendeleo ya familia na taifa. Tunakaribisha jamii, waajiri na wadau kuungana nasi kujenga mfumo wenye heshima, usalama na thamani ya kweli.