Thamani Trust Logo

Wadau na Ushirikiano

Tunajenga mfumo wa mafanikio ya muda mrefu kupitia ushirikiano wa serikali, taasisi za fedha, asasi za kiraia, vyombo vya habari, viongozi wa jamii na sekta binafsi.

Kwa nini Ushirikiano ni Muhimu?

Dhamira ya kulinda hadhi, usalama na haki za dada wa kazi inahitaji nguvu ya pamoja. Kupitia ushirikiano wa kimkakati, Thamani Trust Foundation huunganisha mifumo ya sheria, afya, fedha, elimu na teknolojia ili kujenga mazingira salama ya ajira na ustawi wa familia.

Makundi ya Wadau

Serikali na Taasisi za Umma

  • - Wizara ya Kazi, Vijana na Ajira
  • - OSHA
  • - NSSF, CHF, NHIF
  • - Serikali za Mitaa
  • - WCF - Workers Compensation Fund

Taasisi za Fedha

  • - Benki (CRDB, NMB, NBC na nyingine)
  • - SACCOS na vikundi vya akiba
  • - Taasisi za mikopo midogo

Mawasiliano na Teknolojia

  • - Vodacom, Airtel, Tigo, Halotel
  • - Wadau wa huduma za malipo ya kidijitali
  • - Wadau wa usimamizi wa data na usalama wa taarifa

Asasi, Vyombo vya Habari na Viongozi wa Jamii

  • - NGOs na Asasi za kiraia
  • - Redio, TV, magazeti, mitandao
  • - Makanisa, misikiti na viongozi wa kijamii

Fursa za Ushirikiano

Kuchangia ufadhili wa vitabu, vifaa na mafunzo

Kushiriki kuendeleza mfumo wa kidijitali wa usajili na ufuatiliaji

Kuunga mkono kampeni ya heshima na utu kwa dada wa kazi

Kushiriki tafiti, takwimu na ushawishi wa sera za ajira salama

Jiunge na Harakati ya Sauti ya Thamani

Kama wewe ni taasisi, kampuni, kiongozi wa jamii, au mdau binafsi, unaweza kuwa sehemu ya mabadiliko ya kweli kwa kushirikiana nasi katika mafunzo, ulinzi wa haki, na ustawi wa dada wa kazi Tanzania.